Kiungo wa Manchester United Juan Mata ameelezea jinsi anavyopata tabu toka kwa kiungo wa Arsenal Santi Cazorla baada ya klabu yake kupokea kichapo cha magoli 3-0 jumapili iliyopita.
Mata ambaye yuko na Cazorla katika kikosi cha Hispania kinachojiandaa na michezo ya kufuzu kwa fainali za Ulaya mwakani dhidi ya Ukraine na Luxembourg ameiambia redio Cadena Ser kuwa amekuwa hapumui kutokana na kutambiwa na kiungo huyo wa Arsenal.
Mata amesema "Cazorla amekuwa akilazimisha tukae katika meza moja wakati wa kula ili aendelee kunitania na kunitambia kuhusu kichapo kile.Cazorla ni msumbufu sana"
hahahahaaaa nimeipenda hii
ReplyDelete