Taifa Stars imeanza vyema mbio za kusaka nafasi ya kuingia makundi ya kuwania tiketi ya kombe la dunia Urusi mwaka 2018 baada ya leo jioni kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Malawi katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa,Dar es salaam.
Stars ilipata magoli hayo katika kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wake wawili wanaokipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Congo Mbwana Samatta 18' na Thomas Ulimwengu 22'.
Stars itarudiana tena na Malawi siku ya jumapili huko Blantyire na iwapo Stars itashinda mchezo huo itavaana na Algeria.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Himid Mao, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Hajib dk86, Said Ndemla, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa/Salum Telela dk69 na Farid Mussa/Simon Msuva dk80.
Malawi; Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Mivale Gabeya, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri, Chimango Kayira, Micium Mhone/Mamase Chiyasa dk46, Chawangiwa Kawanda, John Banda/Gabadinho Mhango dk58 na Robin Ngalande.
0 comments:
Post a Comment