728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, October 08, 2015

    CARLOS TEVEZ KURUDI JUVENTUS,BOCA JUNIORS NJAA TUPU

    Turin,Italia.

    Mshambuliaji Carlos Tevez "Apache" huenda akarudi katika klabu yake ya zamani ya Juventus na kuachana na klabu yake ya sasa ya Boca Juniors ya nyumbani kwao Argentina.

    Tevez,31 anafikiria kurudi tena Juventus baada ya Boca Juniors kushindwa kumlipa mshahara kwa kipindi cha miezi mitatu sasa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayoikabili miamba hiyo ya Argentina.

    Lakini taarifa kutoka ndani ya klabu ya Juventus zimasema klabu hiyo haiko tayari kumsajili Tevez kwa mara ya pili hii ni kutokana na nyota huyo kulazimisha kuhama licha ya uongozi kumtaka asifanye hivyo.

    Mpaka sasa Teves ameichezea Boca Juniors jumla ya michezo 12 akiifungia magoli 8 na kutengeneza matatu.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CARLOS TEVEZ KURUDI JUVENTUS,BOCA JUNIORS NJAA TUPU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top