728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, October 08, 2015

    CAFU ATAKA NEYMAR AVULIWE UNAHODHA BRAZIL,HII NDIYO SABABU ALIYOITOA

    Rio de Janeiro,Brazil.

    Mlinzi wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Cafu amemtaka kocha wa timu hiyo Carlos Dunga kumvua kitambaa cha unahodha staa wa timu hiyo Neymar Jr,23 kwasababu jukumu hilo ni kubwa kwake na linamzuia kufanya vizuri uwanjani.

    Cafu amesema kumpa Neymar jukumu kubwa kama hilo ni kama kumfunga kwani unahodha unahusisha mambo mengi sana kwa wakati mmoja.Kucheza na kuongoza wachezaji wenzake kunamfanya Neymar ashindwe kuonyesha kipaji chake kwa asilimia mia moja.

     Amesema "Tunapaswa kumuondolea jukumu hilo na kumuacha afikirie kufunga zaidi.Hapaswi kuwa mtu wa kuongea ongea na marefa kila muda ama kuwa daraja kati ya kocha na wachezaji.

    Neymar ndiyo nembo ya Brazil kwa kipindi hiki,hebu tumuache acheze mpira na siyo kuongoza.Hana uwezo wa kufanya vyote kwa pamoja.Nadhani Miranda na David Luiz wanafaa zaidi kuchukua nafasi hiyo kwani ni viongozi" Alimaliza Cafu.

    Neymar Jr alipewa unahodha na kocha Dunga,Septemba 2014 akichukua nafasi ya mlinzi Thiago Silva.Mpaka sasa Brazil imeshinda michezo 14 kati ya 16 ikiwa na Neymar kama nahodha wake.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAFU ATAKA NEYMAR AVULIWE UNAHODHA BRAZIL,HII NDIYO SABABU ALIYOITOA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top