728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, October 08, 2015

    KOCHA ATAKA KULINUNUA KOMBE ALILOLITWAA MWAKA 1999

    Kocha wa zamani wa klabu ya Parma ya Italia Alberto Malesani anataka kulinunua kombe la UEFA alilolitwaa na klabu hiyo mwaka 1999.

    Malesani anataka kulinunua kombe hilo baada ya Parma kuanza kuuza mali zake ili kuweza kupata fedha za kulipa madeni lukuki iloyonayo klabu hiyo ambayo imeshushwa daraja mpaka Seria D baada ya kufilisika na kushindwa kulipa deni la euro milioni 200.

    Parma ilitwaa taji hilo la UEFA ikiwa na nyota kama Gianluigi Buffon, Lilian Thuram, Fabio Cannavaro, Juan Sebastian Veron, Hernan Crespo na Enrico Chiesa baada ya kuibamiza Marseille magoli 3-0,Mei 12, 1999 huku Moscow.

    Bei ya kuanzia ya taji hilo litakaluzwa kwa njia ya mnada hapo Octoba 12 ni euro elfu 50,000.

    Kwasasa Malesani hana timu baada ya kufutwa kazi na klabu ya Sassuolo mwaka 2014,lakini kumbukumbu yake kubwa inabaki Parma ambapo mbali ya kutwaa taji hilo la UEFA pia alitwaa Coppa Italia na Supercoppa Italiana.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA ATAKA KULINUNUA KOMBE ALILOLITWAA MWAKA 1999 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top