Eriksen ni kiboko.Hii ni kauli ya mlinda mlango wa Swansea City Lukasz Fabianski wakati akimuongelea kiungo wa Tottenham Hotspurs Christian Eriksen.Fabianski ametoa kauli hiyo baada ya kiungo huyo kumfunga magoli mawili ya freek kick (faulo) jumapili iliyopita katika mchezo wa ligi kuu England.
Fabianski amesema "Nilimtazama katika mchezo dhidi ya Manchester City jinsi alivyopiga free kick iliyogonga mwamba na kisha Harry Kane kufunga,nikajua nini cha kufanya lakini bado amenifunga mara mbili.Eriksen ndiye mchezaji wa kwanza kunifunga mara mbili kwa free kick katika mchezo mmoja.Alimaliza Fabianski.
Eriksen ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga magoli kwa mipira ya freek kick (faulo) kwani mpaka sasa amefanikiwa kufunga jumla ya magoli sita tangu ajiunge na Tottenham mwaka 2013 akitokea Ajax ya Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment