YANGA jeuri! Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya uongozi wa timu hiyo kusema pamoja na kuonyesha cheche zao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, bado wanaichukulia ligi hiyo kama mazoezi ya maandalizi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, wameapa kutetea ubingwa wao mapema, huku akili yao ikilenga zaidi kufika mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Itakumbukwa msimu huu, Yanga ilifurukuta kwenye michuano ya kimataifa baada ya kufika hadi raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kabla ya kutolewa na Etoile du Sahel ya Tunisia kwa kipigo cha jumla cha mabao 2-1 baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini.
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, amesema moja ya mikakati yao msimu huu ni kufika mbali katika michuano ya kimataifa.
Alisema wanaipa nafasi ndogo michuano ya ndani ikiwemo Ligi Kuu Bara,wakilenga zaidi kuiandaa timu yao kushiriki vyema michuano ya kimataifa.
Tiboroha alisema wamefanya usajili wa nguvu wa mamilioni ya fedha kutokana na malengo yao hayo kimataifa, lakini pia kutangaza ubingwa wa Bara mapema.
Aliongeza katika kufanikisha malengo yao hayo, tayari wamelitaka benchi la ufundi la timu hiyo kutengeneza programu maalumu kuwaandaa wachezaji tayari kwa michuano ya kimataifa.
(Gazeti la bora la Bingwa)
0 comments:
Post a Comment