728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 21, 2016

    BARCELONA YALAMBA DILI KUBWA TOKA NIKE

    Barcelona,Hispania.

    Klabu ya FC Barcelona imesaini mkataba mpya wa miaka kumi na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike yenye makao yake makuu nchini Marekani.

    Mkataba huo mpya utakaofikia tamati yake mwaka 2026 umeripotiwa kuwa na thamani ya £120m [€155m] sawa na Dola milioni 174 kwa mwaka.

    Kufuatia mkataba huo mpya, FC Barcelona sasa ndiyo Klabu yenye udhamini mkubwa zaidi duniani ikiwa imeutupa mbali ule mkataba wa Manchester United na Adidas wenye thamani ya £75m (Dola 109m) kwa mwaka.

    Nike na FC Barcelona zilianza kufanya kazi pamoja tangu mwaka 1998.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCELONA YALAMBA DILI KUBWA TOKA NIKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top