Evans Aveva
Dar es salaam,Tanzania.
LICHA ya Rais wa Simba, Evans Aveva,kuitisha mkutano Juni 10 mwaka huu,wanachama wa klabu hiyo wanaonekana kumkalia kooni baada ya kuitisha wa kwao utakaofanyika Jumamosi wiki hii, kwa lengo la kujadili mwenendo mbovu wa timu yao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mkutano huo umepangwa kufanyika saa 5 asubuhi katika kata 14 wilayani Temeke,baada ya Simba kushindwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu minne mfululizo.
Akizungumza jana, mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, Hussein Simba,alisema wanatarajia kuwa na kikao na baadaye kutoa uamuzi mzito.
Hussein ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya mashindano wa Simba, alisema wanachama watapata fursa ya kujadili kwa kina mwenendo wa matokeo mabaya kwa timu yao.
Alisema kitendo cha timu yao kufanya vibaya Ligi Kuu na kushindwa kushiriki michuano ya kimataifa kimekuwa kikiwakosesha usingizi hasa kutokana na kejeli za watani wao wa
jadi Yanga.
“Tunataka waandishi wa habari mfike kwenye mkutano wetu wa wanachama kwani tutajadili maendeleo ya klabu yetu,” alisema Hussein.
CHANZO:BINGWA
0 comments:
Post a Comment