Nice,Ufaransa.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Nice Mfaransa Hatem Ben Arfa huenda kwa sasa akawa ndiye mchezaji anayewindwa na vilabu vingi zaidi vya Ulaya ili asajiliwe.
Akiongea na Le Journal du Festival,Ben Arfa mwenye miaka 29 amefichua kuwa mpaka sasa jumla ya vilabu 18 vimeshamfuata kwa lengo la kumshawishi ili ajiunge navyo pindi mkataba wake katika klabu yake ya Nice ukatapokuwa umekwisha hapo Juni 30.
Amesema "Kwa sasa kuna vilabu 18 ambavyo vimeonyesha nia ya kutaka kunisajili lakini mpaka dakika hii nimefanikiwa kuvipunguza na kubaki na vitatu peke yake ambavyo nina hakika ninaweza kujiunga navyo ikiwa nitaamua kuondoka Allianz Riviera.
"Nahitaji kufanya maamuzi sahihi zaidi msimu huu.Nitafikiria kwa kina.Nitashirikisha pia watu wangu wa karibu kabla ya kufanya maamuzi.
Baadhi ya vilabu vinavyodaiwa kumuwania kiungo huyo wa zamani wa Marseille na Newcastle United ni pamoja na Barcelona,Lyon na Paris Saint-Germain.
Ben Arfa amejikuta akiingia katika anga za vilabu mbalimbali baada ya kuifungia Nice mabao 17 katika msimu uliomalizika wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa maarufu kama League 1.
0 comments:
Post a Comment