Hanover,Ujerumani.
Klabu ya Wolfsburg imepata pigo baada ya kiungo wake kinda raia wa Ubelgiji Junior Malanda (20) kufariki kwa ajali ya gari.
Malanda alifikwa na umauti huo jumamosi mchana katika eneo liitwalo Porta Westfalica baada ya gari aina ya Volkswagen Touareg aliyokuwa amepanda kumshinda dereva kutokana na mvua kali na kugonga mti uliokuwa kando kando ya barabara na kupinduka.
Habari zaidi zinasema Maranda aliyekuwa ni abiria katika gari hilo lililokuwa na watu wengine wawili ndani yake alikuwa akielekea uwanja wa ndege wa Hanover kuungana na wachezaji wenzie wa Wolfsburg tayari kwa kambi ya mazoezi huko Afrika ya kusini.
Malanda ambaye msimu huu ameichezea Wolfsburg jumla ya michezo 17 na kuifungia mabao na kutengeneza mengine manne alitua Volkswagen Arena akitokea klabu ya nyumbani kwao Ubelgiji ya Zulte Waregem.
0 comments:
Post a Comment