728x90 AdSpace

Sunday, January 18, 2015

TAARIFA ZOTE MPYA ZA USAJILI ULAYA JUMAPILI TAR 18

De Gea:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuwa tayari kumtoa mlinda mlango wake David De Gea pamoja na kitita cha £50m kwa ajili ya kumsajili nyota wa klabu ya Real Madrid Gareth Bale hapo majira ya kiangazi.

Hummels:Klabu ya Manchester United pia imeripotiwa kusitisha kwa muda mpango wa kuwasajili kiungo Kelvin Strootman na mlinzi Matt Hummels mpaka hapo majira ya kiangazi.

Coquelin:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kujiandaa kumpa mkataba mpya kiungo wangu aliye katika kiwango kizuri kwa sasa Francis Coquelin 23 kabla mkataba wake haujaisha mwezi juni mwaka huu.

Salah:Klabu ya Hull City inajipanga kuwasajili nyota Mohammed Salah na Aaron Lenon ili kujiimarisha katika mbio za ligi kuu England.

Eto'o:Klabu ya Sampdoria iko hatua chache ili kuinasa saini ya mshambuliaji Samweli Eto'o toka klabu ya Everton baada ya kukubali mkataba wa miaka miwili na nusu.

Mirallas:Klabu ya Dortmund imeripotiwa kuanza kumsaka winga wa klabu ya Everton Kelvin Mirallas ambaye amebakiza miezi 18 tu kumaliza mkataba wake Goodson Park.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: TAARIFA ZOTE MPYA ZA USAJILI ULAYA JUMAPILI TAR 18 Rating: 5 Reviewed By: Unknown