728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, January 15, 2015

    ROBBEN:MIMI KUSTAAFU? LABDA MIAKA 10 IJAYO

    Winga wa klabu ya Bayern Munich Arjen Robben amesema suala la yeye kustaafu soka huenda likawa baada ya miaka 10 ijayo.

    Robben ambaye baadae mwezi huu anatimiza miaka 31 akiongea baada ya kumalizika kwa mchakato wa kumpata mchezaji bora wa dunia huko Zurich,Uswisi amesema

    "Nimekuwa nikiulizwa mara nyingi kuhusu kuastaafu,sababu naonekana nazeeka sasa.

    Ilimradi mwili wangu bado uko vizuri na ninafurahia,nitaendelea.Labda mwaka mmoja.Labda miwili,Labda kumi ijayo.Unajua jinsi unavyokua ndiyo unavyozidi kuujua mwili wako vizuri"

    Akiulizwa kuhusu kocha wake Pep Guardiola,Robben amesema...

    "Pep ni kocha bora sana kwani licha ya kwamba amekuwa akiiboresha timu pia amekuwa akijitahidi kumboresha mchezaji mmoja mmoja.

    "Nashukuru kufanya kazi chini yake kwa miezi 18 sasa.Amenifanya niwe bora zaidi,namshukuru kwa hilo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ROBBEN:MIMI KUSTAAFU? LABDA MIAKA 10 IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top