London,England.
Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror klabu ya Arsenal itazikosa kwa muda wa miezi mitatu huduma za mlinzi wake wa kulia Mathew Debuchy kufuatia kuumia bega la mkono wake wa kulia.
Debuchy aliumia bega hilo katika mchezo wa ligi kuu baada ya kusukumwa na kuanguka vibaya na
winga wa klabu ya Stoke City Marko Arnautovic katika mchezo ambao Arsenal iliibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Hili ni pigo kubwa la pili kwa Debuchy ambaye alirejea hivi karibuni baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kufuatia kuumia kifundo cha mguu (ankle).
Kufuatia habari hizo mbaya ripoti zinasema kuwa kocha Arsene Wenger ameahidi kusajili mlinzi mwingine mpya katika dirisha hili la usajili barani Ulaya ili kuimarisha safu yake ya ulinzi.
0 comments:
Post a Comment