Klabu ya Arsenal leo jumatatu inatarajiwa kufungua mazungumzo rasmi na klabu ya As Roma kwa ajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji Mattia Destro 23 ili kuziba pengo lililopo klabuni hapo kufuatia kuondoka kwa Lukas Podolski na Yaya Sanogo.
Klabu ya Arsenal pia imeripotiwa kuanza mazungumzo na klabu ya Villarreal kwa ajili ya kumnasa mlinzi Gabriel Baptista.Inasemekana
Arsenal imetenga £5m kumnasa mlinzi huyo.
Klabu ya Liverpool imeachana na mpango wa kumrudisha kikosini nyota wake aliyeko kwa mkopo katika klabu ya Lille Divock Origi (20) na badala yake itabaki na washambuliaji wake waliopo.
Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Emanuel Adebayor (29) amesema hana mpango wa kuhama klabuni hapo licha ya kutakiwa na vilabu vya Parma na As Milan.
Wamiliki wa klabu ya West ham United David Gold na David Sullivan wamewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa wategemee usajili mwingine mkubwa baada ya ule wa Alex Song.
Klabu ya Real Madrid inapanga kumpiga bei mshambulaji wake Karim Benzema kwenda klabu ya Liverpool kwa £40m ili kupata fedha za kumnunua mshambuliaji wa Psg Edinson Cavani.
0 comments:
Post a Comment