728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 30, 2015

    MPYA ZA IJUMAA KATIKA USAJILI HIZI HAPA

    Anderson:Kiungo wa klabu ya Manchester United Anderson huenda akahama wiki hii baada ya klabu ya Internacional ya nyumbani kwao Brazil leo kuripotiwa kuwa katika mazungumzo mazito ya kumsajili.

    Forlan:Cerezo Osaka imetoa ofa kwa Vilabu vya Hull City na West Bromwich City kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wake Diego Forlan 35.

    Doumbia:Klabu CSKA Moscow imeripotiwa kukubali ofa toka klabu ya As Roma kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake hatari Seydou Doumbia

    Schurrle:Klabu ya Wolfsburg huenda ikatangaza kumsajili winga wa klabu ya Chelsea leo ijumaa baada ya kumaliza kumfanyia vipimo vya afya nyota huyo mshindi wa medali ya dhahabu ya kombe la dunia Andre Schurrle 24 mwenye thamani ya £28m.

    Sinclair:Klabu ya Aston Villa imekubali kumsajili kwa mkopo winga wa klabu ya Manchester City Scott Sinclair mpaka mwisho wa msimu na kisha kumsajili baadae kwa dau £2.5m

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MPYA ZA IJUMAA KATIKA USAJILI HIZI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top