728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, January 15, 2015

    FAHAMU MENGI KUHUSU MICHUANO YA AFCON

    Imeandaliwa na Paul Manjale.

    Tukiwa tumebakiza masaa machache ambayo naona hata uvivu kuyataja tuzishuhudie fainali za 30 za michuano ya kombe la mataifa huru ya Africa maarufu kama (AFCON) hebu tufahamu mengi kuhusu michuano hii inayoanza kutimua vumbi lake tarehe 17 Jan na kumalizika Feb 8 huko Equatorial Guinea.

    .

    Karibu tuanzie hapa,Mwaka 1957 historia iliandikwa
    kwa mara ya kwanza michuano hii ilifanyika mwaka 1957 huko Sudan na kushirikisha jumla ya mataifa matatu tu ambayo ni Misri,Sudan na Ethiopia huku taifa la Afrika ya kusini ambalo lilikuwa lichuane katika michuano hiyo lilienguliwa dakika za mwisho kutokana na kuendekeza sera zake za kibaguzi wakati huo na kuacha ubingwa ukienda Misri.
    Kuanzia mwaka 1968 michuano hii yenye utajiri mkubwa imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka miwili na kushirikisha jumla ya mataifa 16 ambayo hupangwa katika makundi manne ya timu nne nne.Bingwa wa michuano hii huiwakirisha Afrika katika michuano ya kombe la mabara lililo chini ya FIFA.
    Mwaka 1970 historia nyingine  yaandikwa!!
    Miaka 13 baada ya michuano hiyo kuanzishwa huko Sudan, ilirejea tena nchini humo katika jiji la Khartoum ikiwa na sura mpya.Sura ya Kiulaya Ulaya ambapo mashindano hayo kwa mara ya kwanza yalirushwa moja kwa moja yaani "Live" kupitia vituo vya televisheni (Luninga) na kutazamwa sehemu mbalimbali duniani.


    Makubwa!!fainali yapigwa mara mbili kumpata bingwa wa michuano.
    Ilikuwa ni waka 1974 mchezo wa fainali ilibidi uchezwe mara mbili ili kumpata bingwa wa michuano hiyo kwa kuwa wakati huo mikwaju ya penati ilikuwa bado haijaanza kutumika katika soka.

    Je ilikuwaje?
    Mchezo huo wa kukata na shoka wa fainali ulikuwa kati ya Zaire na Zambia ambapo mpaka mwisho matokeo yalikuwa ni sare ya goli 2-2.Magoli ya Zaire yalifungwa na mshambuliaji hatari wakati huo Mulumba Ndaye na Wazambia wakichomoa dakika ya 120 kupitia kwa Brighton Sinyangwe hivyo fainali nyingine kupangwa kurudiwa tena siku mbili baadae.
    Katika mchezo wa marudiano (fainali ya pili) alikuwa ni yule yule muuaji wa Zaire Mulumba Ndaye safari hii tena alifunga mara mbili na kukata ngebe za Wazambia ambao kila dakika ilikuwa ni chungu kwao kutokana na kuushindwa kabisa kuuzima muziki mzito wa Kikongo.
    Je,ni taifa gani linaloongoza kwa kutwaa mara nyingi zaidi taji la michuano hii?
    Misri ndiyo taifa linaloongoza kwa kutwaa mara nyingi ubingwa wa michuano hii.Misri imetwaa michuano hii mara saba ikifuatiwa na  mataifa ya Ghana na Cameroon ambayo yametwaa mara nne,Nigeria mara tatu.Congo Drc mara mbili huku mataifa ya Ivory Coast, Zambia, Tunisia,Sudan, Algeria, Ethiopia, Morocco,Afrika ya kusini na Congo Brazaville yakitwaa ubingwa huo mara moja moja.
    Je,nani ni mfungaji bora wa muda wote??
    Samwel Eto'o wa Cameroun ndiye anayeshikiria rekodi hii baada ya kufunga jumla ya magoli 18 na kuvunja rekodi ya magoli 14 iliyokuwa ikishikiriwa na mshambuliaji hatari wa zamani wa Ivory Coast Laurent Pokou.Eto'o aliweka rekodi hiyo mwaka 2008,

    Je,michezo itapigwa kwenye viwanja gani?
    Michezo yote 32 inatazamiwa kupigwa katika viwanja vinne vya kisasa.Viwanja hivyo ni:
     

    Estadio de Bata ulioko huko Bata wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 35,700.
    Huu ndiyo uwanja mkubwa zaidi nchini Equatorial Guinea ikumbukwe ni moja kati ya viwanja vilivyotumika katika michuano  kama hii hii ya mwaka 2012 iliyofanya kwa ushirikiano kati yake na Gabon.Uwanja huu hutumika kwa mpira wa miguu na riadha

    Nuevo Estadio de Malabo ulioko huko Malabo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 15,250.
    Huu ndiyo uwanja wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea ambao ulitumika pia katika michuano ya mwaka 2012.
    Uwanja huu pia hutumika kama uwanja wa nyumbani kwa vilabu sita vya ligi ya nchi hiyo maarufu kama  "Equatoguinean".Vilabu hiyo ni Atletico Malabo,Atletico Semu,Deportivo Unidad, Sony Ela Ngueman,The Panthers na  Vegetarianos.

    Estadio de Mongomo ulioko huko Mongomo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 15,000.
    Uwanja huu ulioko huko Mongomo pembezoni sana mwa nchi hiyo hutumika kwa michezo ya aina zote (Multi-purpose).

    Ebebiyin – Nuevo Estadio de Ebebiyin (Uwezo,Watazamaji 5,000):
    Uwanja huu uko katika mji wa  Ebebiyin ambao upo karibu kabisa na mipaka ya nchi tatu za  Equatorial Guinea,
    Gabon na Cameroon.

    Je ni mataifa gani yanayopewa nafasi kutwaa ubingwa wa michuano ya mwaka huu?
    Kama ilivyo kawaida watu mbalimbali wamejaribu kutoa utabiri wao kuhusu taifa ambalo litatwaa ubingwa huo.Mataifa yanayopewa nafasi kubwa ni pamoja na Ivory Coast,Ghana na Algeria.

    Je,makundi yenyewe yakoje?
    Kundi A-Equatorial Guinea,Burkina Faso,Gabon na Congo.
    Kundi B-Zambia,Tunisia,Cape Verde na Congo DRC.
    Kundi C-Ghana,Algeria,Afrika Kusini na Senegal
    Kundi D-Cote d'Ivoire,Mali,Cameroon na Guinea
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FAHAMU MENGI KUHUSU MICHUANO YA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top