728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, January 22, 2015

    MPYA ZOTE ZA LEO ZA USAJILI ZIKO HAPA

    Eto'o:Klabu ya New York Cosmos inajipanga kuizidi ujanja klabu ya Sampdoria kwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Everton Samwel Eto'o katika dirisha hili la usajili.Iwapo Eto'o atatua Cosmos atakuwa pacha wa nyota wa zamani wa Real Madrid Raul Gonzalez.

    Baptista:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuingia katika mbio za kumnasa mlinzi wa Villarreal ambaye pia anasakwa na Arsenal Gabriel Baptista.

    Salah:Klabu ya As Roma imeripotiwa kumtaka kwa mkopo wa miezi sita winga wa klabu ya Chelsea Mohammed Salah na baadae kumsajili jumla kwa ada ya £12m.

    Anderson:Kiungo wa klabu ya Manchester United Anderson ataendelea kubaki klabuni hapo mpaka mkataba wake utakapoisha mwezi julai baada ya kukosa ofa toka klabu yoyote.

    Jenkinson:Klabu ya Arsenal imeiambia klabu ya Westham kama inataka kumsajili moja kwa moja mlinzi wake aliyeko klabu hapo kwa mkopo Carl Jenkinson 22 ijiandae kutoa dau la £12m

    .Chelsea:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuendelea na mikakati ya kutaka kujiimarisha zaidi baada ya kuripotiwa kutenga kitita cha £68m kwa ajili ya kuwanasa nyota wawili wanaotamba katika ligi ya Seria A Juan Quadrado na Paul Pogba.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MPYA ZOTE ZA LEO ZA USAJILI ZIKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top