Bata,Guinea.
Michuano ya 30 ya kuusaka ubingwa wa Afrika (AFCON) imeanza kutimua vumbi lake nchini Equatorial Guinea kwa michezo miwili ya kundi A iliyopigwa katika dimba la Estadio de Bata.
Katika mchezo wa mapema wenyeji Guinea walishindwa kuutumia vizuri uenyeji wao baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Congo Brazzaville.Bao la Guinea limefungwa na Emilio Ensue huku lile la Congo likifungwa na Thievy Bifouma.
Katika mchezo wa pili licha ya Burkina Faso kutawala sehemu kubwa ya mchezo lakini walijikuta wakiangukia pua baada ya kufungwa bao 2-0 na vijana wa Gabon.Magoli ya Gabon yalifungwa na nahodha Pierre Emerick na Malick Evouna.
Leo tarehe 18 ni zamu ya kundi B
Zambia v Congo DR
Tunisia Cape Verde Islands
0 comments:
Post a Comment