Manchester, England.
Kiungo wa klabu ya Manchester City Mfaransa Samir Nasri amefichua kwamba kocha Alex Ferguson alishindwa kumshawishi vizuri ili ahamie Manchester United. Nasri aliyejiunga na Manchester City mwaka 2011 akitokea klabu ya Arsenal amesema aliyekuwa kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson alimwambia kwamba anataka kumsajili lakini alimpa sharti la kuhakikisha kwanza anaingia vitani na klabu yake ya Arsenal wakati huo.
Akifanya mahojiano na kituo cha IBein Nasri amesema "Tulikutana Ufaransa kwa siri katika nyumba binafsi. Hatukutaka kufanyia mazungumzo yetu hotelini kwa kuogopa kuonekana. Ferguson alinitamkia kuwa anataka kunisajili lakini kukatokea tatizo moja. Aliniambia kuwa hajawahi kusajili mchezaji kutoka Arsenal hivyo alinitaka niingie kwanza vitani na Arsenal ndipo yeye apate kunisajili.
Sikuona sababu ya kufanya hivyo. Sikutaka kuingia vitani na Arsenal hasa Arsene Wenger hivyo nilikataa na hatimaye nikaamua kujiunga na Manchester City.
0 comments:
Post a Comment