Barcelona,Hispania.
Klabu ya Barcelona imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya leo kuichapa klabu ya Derpotivo la Coruna kwa jumla ya magoli 4-0.Hii ni hat-trik ya 22 ya Messi akiwa na Barcelona.
Ikicheza ugenini Barcelona ilijipatia magoli yake kupitia kwa mshambuliaji wake nyota aliyefunga magoli matatu (hat-trik) huku mlinzi wa Derpotivo Sidinei akifunga katika harakati za kuokoa.
Kufuatia ushindi huo Barcelona imeendelea kubaki katika nafasi ya pili ikiwa ni pointi moja pungufu ya vinara Real Madrid ambao katika mchezo uliopigwa mapema waliitandika Getafe kwa jumla ya magoli 3-0.
Magoli ya Madrid yamefungwa na Cristian Ronaldo aliyefunga mara mbili huku Gareth Bale akifunga moja.
Katika mchezo mwingine wa La Liga uliopigwa huko Vicente Calderon wenyeji Atletico Madrid wameifunga Granada kwa jumla ya magoli shukrani za dhati ziende kwa mshambuliaji Mario Mandzukic aliyefunga moja na kiungo Raul Garcia aliyefunga moja.
0 comments:
Post a Comment