Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi usajili wake wa kwanza wa dirisha dogo baada ya kumsajili kinda wa Kipoland Kyristin Bielk toka klabu ya Legia Warsaw kwa ada inayodhaniwa kuwa ni £2.5m.
Bielk 17 alijiunga na Warsaw mweni julai mwaka 2014 akitokea klabu ya Lech Poznan na kufanikiwa kucheza jumla ya michezo sita na kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ukiwemo mmoja wa ligi ya Europa.
Bielk ambaye kiuchezaji anafananishwa na kiungo wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji pamoja na mlinzi wa kati.
0 comments:
Post a Comment