Bielik:Klabu ya Arsenal leo inatarajiwa kumfanyia vipimo vya afya kiungo kinda wa ulinzi Krystian Bielik (17) toka klabu ya Legia Warsaw ya Poland kabla ya kumsajili kwa dau la £2.5m.
Neil Tylor:Klabu ya Swansea imekataa ofa ya £3m toka klabu ya Crystal Palace kwa ajili ya mlinzi wake wa kushoto Neil Tylor.
Adebayor:Klabu ya As Roma
imeripotiwa kuwa katika mawindo ya kumsajili mshambuliaji anayesugua benchi Tottenham,Emanuel Adebayor.
Klabu ya Southampton ipo karibu kuinasa saini ya kiungo wa Braga Rafa Silva 22 kwa ajili ya kuimarisha matumaini yake ya kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.
Manchester United:Leo ijumaa ndani ya viunga wa klabu ya Manchester kutakuwa na kikao kizito kati ya kocha wa klabu hiyo Luis Van Gaal na maafisa wa juu wa klabu hiyo kujadili kama timu inahitaji kusajili wachezaji wapya dirisha hili ama la.
Marco Reus:Klabu ya Real Madrid imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili winga wa klabu ya Dortmund Marco Reus kwa €28m na mkataba wa miaka mitano hapo majira ya joto.
Mourinho:Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Chelsea zinasema kocha mkuu wa klabu hiyo Jose Mourinho anajipanga kuwasajili nyota wawili wa klabu ya Real Madrid Jese Rodriguez na Raphael Varane kwa kitita cha €48m.
Higuain:Wakala na kaka wa mshambuliaji Gonzalo Higuain amekana kufanya mazungumzo yoyote ya usajili na klabu ya Liverpool na kusisitiza kuwa mteja wake bado ana furaha kuwepo Napoli.
Wenger:Baada ya kukumbwa na majeruhi kocha Arsene Wenger amewaambia wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa anataka kuongeza wachezaji wawili kikosini katika dirisha hili la usajili.
Gomis:Wakala wa mshambuliaji wa klabu ya Swansea City Batefimbi Gomis aitwaye Francesco Di Frisco amesema amefanya mazungumzo na klabu ya Arsenal kuhusu usajili wa mteja wake huyo mwenye thamani ya £6m
0 comments:
Post a Comment