Barcelona,Hispania.
Vilabu vya Barcelona na Real Madrid vimeendelea kuchuana vikali katika mbio za kuusaka ubingwa wa konbe la La Ligo baada ya leo jumamosi kuibuka na ushindi katika viwanja vyao ugenini.
Barcelona iliyokuwa katika dimba la Estadio Manuel Martinez Valero imeibamiza klabu ya Elche kwa jumla ya magoli 6-0 kwa magoli ya Lionel Messi (2),Neymar (2),Pedro (1) na Gerrard Pique (1).
Katika mchezo mwingine Real Madrid imeibanjua klabu ya Cordoba kwa jumla ya magoli 2-1 kwa magoli ya Karim Benzema na Gareth Bale huku Cristian Ronaldo akilimwa kadi nyekundu kwa kugombana uwanjani.
0 comments:
Post a Comment