Ramos:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kufanya mazungumzo na wakala wa mlinzi wa klabu ya Real Madrid Sergio Ramos 28 kwa ajili ya kumsajili mwisho wa msimu.
Rugani:Baada ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Villareal Gabriel Paulista klabu ya Arsenal imeripotiwa kutaka kuongeza mlinzi mwingine na safari hii imehusishwa kumfukuzia mlinzi wa klabu Empoli Daniele Rugani 20.
Lavezzi:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kuwa karibu kutoa kiasi cha €20m kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint Germain Ezequiel Lavezzi.
Mbiwa:Klabu ya As Roma imemsajili moja kwa moja mlinzi wa klabu ya Newcastle Mapou Yanga-Mbiwa 26 kwa ada ya €7.35m baada ya kufanya vizuri klabuni hapo wakati wa uhamisho wake wa mkopo.
Zaha:Kutoka ndani ya klabu ya Crystal Palace taarifa zinasema klabu hiyo iko katika hatua nzuri za kumnasa winga wa klabu ya Manchester United aliyeko klabuni hapo kwa mkopo Wilfred Zaha kwa ada ya £3m.
Nani:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kutaka kumuuza moja kwa moja kwa klabu yoyote winga wake Mreno Louis Nani ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Sporting Cp.
0 comments:
Post a Comment