728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, January 19, 2015

    MOURINHO:CHELSEA MUHESHIMUNI STEVEN GERRARD

    London,England.
    Mourinho akifafanua jambo
    Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amewataka mashabiki wa klabu hiyo kumuheshimu kiungo wa Liverpool Steven Gerrard wakati wote wa mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa kombe la Capital One  utakao vikutanisha vilabu hivyo kesho jumanne.

    Mourinho ametoa rai hiyo baada ya
    mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kumkejeri kiungo huyo kutokana na tukio lake la kuteleza na hatimaye kusababisha goli la pili lililofifisha klabu ya Liverpool kulikosa taji la kwanza la ligi ya Epl.Katika mchezo huo Liverpool ililala kwa magoli mawili bila.

    Mourinho amesema "Najua mashabiki wa klabu yangu wamekua wakimtania Gerrard kutokana na tukio la kuteleza.

    Wana wimbo pia unao mkejeri,kitu ambacho sikipendi kabisa.Wanapaswa kumuheshimu kwa kuwa ni mchezaji wa kihistoria pia ni mchezaji wa kihistoria wa ligi ya England.
    Pia Mourinho ameenda mbali zaidi na kufichua kuwa aliwahi kumtaka kiungo huyo mwaka 2005 ili kuja kuimarisha safu yake ya kiungo iliyokuwa na viungo kama Frank Lampard na Claude Makelele.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MOURINHO:CHELSEA MUHESHIMUNI STEVEN GERRARD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top