Madrid,Hispania.
Klabu ya Barcelona imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi klabu ya Atletico Madrid katika mchezo mkali wa Copa Del Rey uliopigwa usiku wa kuamkia leo alhamisi katika dimba la Vicente Cardelon.
Katika mchezo huo uliojaa ubabe mwingi ilishuhudiwa wenyeji Atletico wakimaliza pungufu baada ya nyota wake wawili Raul Garcia na Mario Suarez kulimwa kadi kadi nyekundu baada ya kuonyesha mchezo usio wa kiungwana.
Magoli ya Atletico Madrid yalifungwa na Fernando Torres na Raul Garcia aliyefunga kwa njia ya penati huku Barcelona ikipata magoli kupitia kwa Neymar Dos Santos aliyefunga magoli mawili na moja la kujifunga wa mlinzi wa Atletico Madrid Joao Miranda.
Kufuatia ushindi huo wa jumla ya magoli 4-2 Barcelona imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe hilo la pili kwa umaarufu nchini Hispania.
0 comments:
Post a Comment