Dar es salaam,Tanzania.
Vilabu vya Simba Sc na Azam Fc vimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa jioni ya leo katika dimba la uwanja wa taifa.
Simba ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Mganda Emanuel Okwi kabla ya Kipre Tchetche kusawazisha kufuatia kazi nzuri ya kiungo Mcha Hamis.
Mchezo huo uliingia nuksi baada ya Emanuel Okwi kupoteza fahamu na kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kufanyiwa madhambi na mlinzi wa Azam Aggrey Morris katika kipindi cha pili.
Matokeo haya ya yamewabakisha Azam
FC kileleni mwa Msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 21 katika mechi 11 wakifuatiwa na Yanga
SC wenye pointi 18 katika mechi 10 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 17 baada ya kushuka dimbani mara 10 huku Simba SC ikiwa na pointi zake 13.
Matokeo mengine ya VPL ni kama ifuatavyo....
Mbeya City 2-2 Prison
Ruvu JKT 2-1 Mtibwa Sugar
0 comments:
Post a Comment