728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 31, 2015

    USAJILI:MRITHI WA GERRARD HUYU HAPA,BAYERN YAMKATAA REUS

    Gignac:Vilabu vya Arsenal na Liverpool vimeripotiwa kuwa katika mchuano mkali wa kumuwania mshambuliaji mahiri Marseille Andre-Pierre Gignac 29 ambapo mwezi juni atakuwa mchezaji huru.

    Dragovic:Mlinzi wa klabu ya Dynamo Kiev Aleksandar Dragovic aliyekuwa akiwindwa vikali na klabu ya Manchester United ameripotiwa kuwa karibu kutua katika klabu ya Inter Milan inayoundwa upya na kocha Roberto Mancini.

    Koem:Kocha mkuu wa klabu ya Southampton Ronald Koeman ameripotiwa kuwa mbio kukiimarisha kikosi chake kwa kuwasajili nyota Tonny Vilhena kutoka klabu ya  Feyenoord kwa ada ya £4m na Filip Djuricic kwa uhamisho wa mkopo toka klabu ya Benfica kwa ajili ya kukata tiketi ya michuano ya Ulaya msimu ujao.

    Batalla:Klabu ya Real Madrid inasemekana imefikia makubaliano ya kumsajili mlinda mlango wa klabu ya River Plate Augusto Batalla na usajili huo utatangazwa wikiendi hii.

    Stindl:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kumfuatilia kwa karibu kiungo na nahodha wa klabu ya Hannover Lars Stindl 26 ili kuwa mrithi wa nahodha wake anayeondoka Steven Gerrard.

    Fletcher:Klabu ya Westham muda wowote kuanzia sasa itamtangaza kiungo wa klabu ya Manchester United Darren Fletcher 30 kuwa mchezaji wake mpya baada ya kumfanyia vipimo vya afya jana ijumaa.

    Reus:Klabu ya Bayern Munich imesema haina mpango wa kumsajili winga wa klabu ya Borussia Dortmund Marko Reus 25 kutokana na kuumia mara kwa mara.Hata hivyo habari hiyo imegeuka faraja kwa vilabu vya Arsenal,Real Madrid na Manchester United ambavyo vilikuwa na hofu ya kuzidiwa ujanja na miamba hiyo ya Bundesliga katika kuipata saini ya nyota huyo mwenye kipaji cha kipekee.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:MRITHI WA GERRARD HUYU HAPA,BAYERN YAMKATAA REUS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top