Neto: Klabu ya Liverpool inajiandaa kutuma ofa ya £2m kwa ajili ya kumnasa mlinda mlango wa klabu ya Fiorentina ya Italia Mbrazil Neto (26).
Lukas: Klabu ya Liverpool pia imeripotiwa kujiandaa kuikataa ofa ya £7m toka klabu ya Inter Milan kwa ajili ya kiungo wake Lukas Leiva kwa madai kuwa ni kiduchu mno.
Schneiderlin: Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuungana na Arsenal katika mbio za kumuwania kiungo wa klabu ya Southampton Morgan Schneiderlin mwenye thamani ya £25.
Mkhitaryan: Klabu ya Juventus ya Italia imeripotiwa kuanza mipango ya chini chini ili kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Borrussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan.
Okazaki:Klabu ya Leceister City imegonga mwamba katika jitihada zake za kumtaka staa wa Kijapani Shinji Okazaki baada ya klabu yake ya Mainz kukataa ofa ya €10m.
Laporte: Klabu ya Manchester United pia imeripotia kuwa karibu kumsajili mlinzi wa kati wa klabu ya Atletico Bilbao mwenye thamani ya £25m Aymeric Laporte 20.
Wenger: Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema ataingia sokoni kusajili mlinzi mwingine baada ya mlinzi wake Mathew Debuchy kuteguka bega.Walinzi wanaotajwa kujiunga na Arsenal ni Loic Perrin wa klabu ya Saint Entieni na Winston Reid wa West ham United.
0 comments:
Post a Comment