Dar es Salaam.
Ziara ya klabu ya Yanga
iliyopangwa kufanyika Zambia mwezi huu kwa maandalizi ya mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya BDF ya Botswana imetoweka.
Safari hiyo ya mechi za kirafiki imefutika baada ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuingilia kati na kuwaalika wenyeji wao, Zesco
kwa mechi za kirafiki.
Kiongozi mwandamizi wa klabu hiyo amesema, Zesco waliokuwa wenyeji wao wamepata mwaliko wa TP Mazembe ili washiriki
mashindano mafupi yatakayoshirikisha pia Azam FC ya Tanzania.
Alisema kiongozi huyo kuwa, kutokana na mabadiliko kwenye safari hiyo,wanaangalia njia nyingine ya kuipa mazoezi timu yao kabla ya kuikabili BDF XI mwezi ujao.
“Zesco walitualika kushiriki mashindano yao mafupi kuanzia Januari 28 hadi Februari 4, ila, nao wamealikwa kule DR Congo, hivyo sisi tumeona tuvunje safari
kwani wenyeji wetu hawatakuwapo,”alisema.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas
Tiboroha alithibitisha kufutwa kwa ziara hiyo na kueleza kuwa timu hiyo itaendelea na mechi za ligi kabla ya kuwavaa.Wabotswana.
“Kweli safari yetu ya Zambia
haitakuwapo na sasa tunaendelea na ligi, kwani wenyeji wetu ambao ndiyo
tulikuwa tuwe nao nchini mwao,
wamepata mwaliko wa TP Mazembe,”alisema.
Yanga ilipanga kuweka kambi ikiwa mgeni wa Zesco ili kujiandaa na mchezo wa kwanza wa michuano ya CAF dhidi ya BDF XI ya Botswana utakaofanyika Februari 14 jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment