728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, January 28, 2015

    KASEJA KIZIMBANI FEBRUARI 12

    Kipa wa Yanga, Juma Kaseja kupitia kwa wakili wake, Samson Mbamba, jana amesomewa shtaka lake kwa mara ya kwanza la kuvunja mkataba kwenye Mahakama ya Kazi.

    Kesi hiyo itaunguruma tena Februari 12 na Yanga wanataka Kaseja awalipe Sh340 milioni ikiwa ni ada ya usajili, ambayo ni Sh40 milioni pamoja na fidia ya Sh300 milioni, ambazo ni gharama za usumbufu wa kuvunja mkataba, kumhudumia na kutunza kiwango chake kwa kipindi chote alichokuwa Yanga.

    Yanga inawakilishwa na mwanasheria wao, Frank Chacha, ambaye alifungua kesi hiyo Ijumaa iliyopita amesema kuwa wamefikia uamuzi huo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine
    kuheshimu mikataba yao.

    Kaseja aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya Novemba 11 mwaka jana, kuandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya kukiuka makubaliano ya mkataba kati yao,akishinikiza kulipwa Sh20 milioni za usajili alizokuwa anaidai klabu hiyo.

    Kaseja kupitia Kampuni ya Mbamba Advocate, iliandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa amekuwa akisugua benchi.

    Pia, uongozi wa Yanga umekiuka makubaliano baina ya pande mbili ambazo hadi Januari mwaka jana walitakiwa kummalizia ada yake ya usajili Sh20 milioni, lakini hata hivyo,haikufanya hivyo hadi alipowasilisha barua ya kuvunja mkataba.

    Akizungumza Wakili wa Kaseja, Samson Mbamba alisema:

    “Tutasimama kizimbani hakuna shida,wala hatubabaishwi na lolote, naamini mteja wangu ana haki  zote, mbivu na mbichi zitajulikana.”

    Kwa upande wake, kipa huyo wa zamani wa Simba, Kaseja alisema hana la kusema kwa sasa na kila kitu amekiacha
    mikononi mwa wakili wake.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KASEJA KIZIMBANI FEBRUARI 12 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top