Mshambuliaji wa Azam,John Bocco ‘Adebayor’ amekwenda
Algeria kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.
Bocco aliyerejea kwenye timu yake ya Azam hivi karibuni baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti na alifanya vizuri na timu hiyo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi
yaliyomalizika mwanzoni mwa wiki na Simba kutwaa ubingwa.
Mchezaji huyo yuko Algeria katika klabu ya Chabab Riadhi Baladiyat (CRB) akifanya majaribio huku klabu hiyo
ikitaka kumnunua moja kwa moja kama itaridhika naye.
Mshambuliaji huyo alikwenda katika klabu hiyo ya Ligi Daraja la kwanza mwanzoni mwa wiki hii na inaelezwa kuwa timu hiyo inataka kumnunua moja kwa moja mchezaji huyo mwenye umbo kubwa na anayejua kufunga mabao ya vichwa.
Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba alisema kuwa wanasubiri majibu ya klabu hiyo kuhusu mchezaji huyo na waliwapa muda hadi leo jioni
kabla ya kuamua vinginevyo.
“Ni kweli Bocco yuko Algeria, kuna timu imetaka kumnunua, lakini walisema wanataka kumwona kwanza na bado
tunasubiri majibu yao na tunawapa hadi kesho(leo) jioni wawe wameshatuambia nini kinaendelea,” alisema Kawemba.
Bocco aliwahi kufanya majiribio kwenye klabu ya Supersport ya Afrika Kusini na kufuzu, lakini hata hivyo Azam iligoma kumuuza kutokana na madai kuwa walipewa fedha kidogo.
0 comments:
Post a Comment