Moreno:Vilabu vya Tottenham na Arsenal vinachuana vikali kuiwania saini ya mlinzi wa kati wa Espanyol raia wa Mexico Hector Moreno (27) ili kuimarisha safu zao za ulinzi.
Enrique:Klabu ya Crystal Palace inajipanga kufanya usajili wa mkopo wa miezi sita wa mlinzi aliyekosa nafasi katika kikosi cha Liverpool Jose Enrique (29).
Cisse:Klabu ya Swansea City inapanga kumsajili mshambuliaji Demba Cisse (29) toka klabu ya Newcastle kwa ada ya £7m ili kuchukua nafasi ya Wilfred Bony aliye njiani kutua klabu ya Manchester City.
Delph:Klabu ya Liverpool inapanga kumsajili kiungo wa Aston Villa Fabian Delph kabla haijamuachia kiungo wake Lukas Leiva anayewindwa na klabu ya Napoli ya Italia.
Defoe:Vilabu vya Sunderland na Toronto Fc vimekubali kubadilishana wachezaji Jozy Altizore na Jermain Defoe (32).Defoe atatoka Toronto kwenda Sunderland.
Carvalho:Klabu ya Arsenal inadaiwa kuwa iko karibu kuinasa saini ya kiungo William Carvalho (22) toka klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno kwa ada ya £25m.
Eto'o:Klabu ya Samporia ya Italia ina matumaini ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Everton Samuel Eto'o baada ya kukubaliana maslahi binafsi.
Song:Klabu ya West ham imeripotiwa kuwa tayari kumpa mkataba wa kudumu kiungo Alex Song aliyeko klabuni hapo kwa mkopo akitokea klabu ya Barcelona.
0 comments:
Post a Comment