728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, January 13, 2015

    USAJILI:STOKE YAMGEUKIA DZEKO,LIVERPOOL YAUZA TENA

    Assaidi:Klabu ya Liverpool imekubali kumuuza winga wake raia wa Morocco Oussama Assaidi (26) kwa dau la £4.5m kwenda klabu ya Al Ahli ya Dubai.

    Balotelli:Klabu ya Jeventus imekana kuwa haiko katika mazungumzo yoyote na klabu ya Liverpool kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Mario Balotelli.

    Dzeko:Klabu ya Stoke City inajipanga kujaribu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Edin Dzeko ambaye huendi asipate namba baada ya klabu hiyo kuwa njiani kumsajili mshambuliaji wa Swansea City Wilfred Bony.

    Sanogo:Klabu ya Arsenal imekubali kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Yaya Sanogo kwenda Crystal Palace mpaka mwisho wa msimu.

    Adebayor:Klabu ya Parma ya Italia imeripotiwa kufanya mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Emanuel Adebayor lakini mshahara wake wa £100,000 kwa wiki umeonekana kuwa tatizo kwa miamba hiyo ya Seria A.

    Reid:Kocha wa West ham Sam Alladyies anasema atamshawishi mlizi wake Winston Reid (27) aachane na mpango wa kuhama klabuni hapo.Reid anawaniwa na vilabu ya Arsenal na Liverpool.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:STOKE YAMGEUKIA DZEKO,LIVERPOOL YAUZA TENA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top