728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 24, 2015

    MPYA ZA USAJILI JUMAMOSI YA LEO HIZI HAPAAA

    Quadrado:Kocha mkuu wa klabu ya Fiorentina Vicenzo Montella ametishia kuikacha timu hiyo ikiwa uongozi utakubali kumuuza winga Juan Quadrado kwenda klabu ya Chelsea katika dirisha hili la usajili.Montello anamuona Quadrado kuwa ni mtu sahihi wa kuipeleka Fiorentina katika kinyang'anyiro cha ligi ya mabingwa msimu ujao kwa sasa Fiora wako nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya Seria A.

    Paulista:Taarifa kutoka Hispania zinadai kuwa klabu ya Villarreal imemuondoka katika kikosi chake kitakachoivaa klabu ya Levante leo mlinzi Gabriel Paulista 24 ili kuangalia uwezekano wa kutimkia England katika vilabu vya Arsenal na Manchester United.

    Eto'o:Klabu ya Sampdoria leo jumamosi inatarajia kumfanyia vipimo vya afya mshambuliaji wa Everton Samweli Eto'o kabla ya kumtangaza rasmi kuwa nyota wake mpya.

    Salah:Klabu ya As Roma iko karibu kabisa kuisana saini ya winga klabu ya Chelsea Mohammed Salah kwa mkopo wa miezi 18 baada ya kufikia makubaliano rasmi.

    Fletcher:Kiungo Darren Fletcher huenda akaikacha klabu yake ya Manchester United na kujiunga na vilabu vya Westham,Valencia na West Bromwich Albion baada ya kukosa namba katika kikosi cha Luis Van Gaal.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MPYA ZA USAJILI JUMAMOSI YA LEO HIZI HAPAAA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top