Dar es Salaam.
Klabu ya Simba imethibitisha kuachana na kocha msaidizi
wa timu hiyo, Seleman Matola na kueleza kumweka hadharani mrithi wake atakayesaidiana na kocha mkuu, Goran Kopunovic wakati wowote kuanzia sasa.
Mapema jana, Rais wa Simba, Evance Aveva alieleza kupokea barua ya kujiuzulu kwa Matola na kubainisha kuwa katika barua hiyo,Matola ameeleza kutingwa na majukumu ya kifamilia hivyo hawezi kuendelea kuinoa Simba kama kocha msaidizi.
Alipotafutwa kuzungumzia
uamuzi wake huo, Matola alitaka aulizwe vizuri Aveva ndiye alitolee ufafanuzi suala hilo na si yeye kwani tayari ameachana na klabu hiyo.
Hata hivyo, kocha huyo alionekana kupoteza mvuto kwa baadhi ya mashabiki ambao mara kadhaa wamekuwa wakimshinikiza ang’atuke Simba.
Kwa mujibu wa Aveva, Simba imepokea barua ya kujiuzulu kwa kocha huyo juzi ikiwa ni siku moja baada ya Simba kuruhusu kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment