728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, January 21, 2015

    COPA DEL REY:LEO NI BARCA vs ATL MADRID

    Uchambuzi na King
    MUDA: Saa 6 usiku.
    Leo katika dimba la Nou Camp jijini Barcelona kutakuwa bonge moja la mechi ya wababe wa La Liga Barca vs A.Madrid.
    Msimu uliopita , Diego Simeone aliiongoza Atletico Madrid kumaliza ngebe za Barca
    na Real za kutwaa Ubingwa wa Spain kwa Miaka 10 baada ya kutoka Sare 1-1 na Barca Uwanjani Nou Camp katika Mechi ya mwisho ya La Liga na wao kutwaa Ubingwa .
    Kwenye Raundi iliyopita ya Copa del Rey Wiki iliyopita , Atletico Madrid waliwabwaga
    Mahasimu wao wakubwa Real Madrid,ambao ndio walikuwa Mabingwa Watetezi , kwa Jumla ya Bao 4-2 katika Mechi mbili.
    Atletico waliishinda Real Mechi ya kwanza 2-0 Nyumbani kwao Vicente Calderon na kutoka Sare 2-2 huko Santiago Bernabeu.
    Hata hivyo , Barcelona iliifumua Elche kwa jumla ya bao 9-0 kwenye Copa del rey  na  kuwabamiza Atletico  Bao 3- 1
    huko Nou Camp kwenye Mechi
    ya La Liga Mapema Mwezi huu .
    Licha ya kipigo hicho , Diego Simeone, Raia wa Argentina , ametamba kuibamiza Barca  kwenye mchezo wa leo .
    Kwa ujumla huu ni mchezo ambao kila timu itakuwa ikihitaji kushinda ili kujiweka vizur kabla ya mechi ya marudiano hapo baadae.
    ...Subir dk90 uone vitu vitamu..
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPA DEL REY:LEO NI BARCA vs ATL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top