London,England.
Klabu ya Chelsea huenda ikazikosa hudumu za mshambuliaji wake Diego Costa kwa majuma matatu baada ya chama cha soka nchini England kuamua kumshitaji kutokana na madhambi aliyomfanyia kiungo wa klabu ya Liverpool Emre Can katika mchezo wa jana jumanne wa kombe la Capital One.
Costa alimkanyaga kwa maksudi Emre Can mapema kabisa mwa kipindi cha kwanza hata hivyo hakuadhibiwa kwa kosa hilo kwa kuwa mwamuzi hakuona tukio hilo.
Baada ya kupitia mkanda wa video wa mchezo huo,FA imeamua kumshitaki Costa kwa kosa hilo pekee huku madhambi mengine aliyomfanyia mlinzi Martin Skrtel yakiachwa.
Costa amepewa mpaka kesho jioni (alhamisi) kutoa utetezi wake kabla ya FA haijachukua hatua za kinidhamu kwa nyota huyo Muhispania ambapo inatarajiwa atakosa michezo mitatu akianza na mchezo wa jumamosi hii dhidi ya Manchester City kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Everton na Aston Villa.
0 comments:
Post a Comment