Klabu ya Bayern Munich imeuanza vibaya mzunguko wa pili wa ligi ya Bundesliga baada ya hapo jana usiku kukubali kipigo cha goli 4-1 toka kwa VFL Wolfsburg.
Wolfsburg ikicheza vizuri na kwa kujituma nyumbani mbele ya mashabiki wake ilipata magoli yake kupitia kwa mshambuliaji Bas Dost aliyefunga mawili (4, 45) na kiungo De Bruyne aliyefunga mawili pia (53,73),wageni Bayern wakijifuta machozi kwa goli la mlinzi Juan Bernat dakika ya 55.
Kufuatia ushindi huo Wolfsburg imeendelea kujikita katika nafasi ya pili katika ligi ikifikisha alama 37 nyuma ya Bayern iliyo na alama 45 katika nafasi ya kwanza.
Vikosi vilikuwa hivi.......
WOLFSBURG: Benaglio, Naldo, Rodriguez,Knoche, Gustavo, Perisic (Schafer 81),Vierinha, Calgiuri (Hunt 86), De Bruyne,
Arnold, Dost (Bendtner 83)
BAYERN MUNICH:Neuer Boateng, Alaba,Rode (Weiser 51), Dante, Robben,Schweinsteiger, Alonso, Bernat, Muller (Gotze
71), Lewandowski (Pizarro 71)
Ratiba ya mechi za leo iko kama ifuatavyo.....
Freiburg v Eintracht Frankfurt Hamburger SV v FC Cologne Mainz 05 v Paderborn
Schalke 04 v Hannover 96
VfB Stuttgart v Borussia Moenchengla
Bayer Leverkusen v Borussia Dortmund
0 comments:
Post a Comment