Zurich,Uswisi.
Winga wa klabu ya Manchester United Muargentina Angel di Maria amevunja ukimya juu ya tuzo za mchezaji bora wa dunia (Ballon d'or) na kutaka kuwepo na mabadiliko ili kutoa nafasi kwa nyota wengine pia kutwaa tuzo hiyo.
Di maria ambaye alikuwa mmoja kati ya mashuhuda wa kinyang'anyiro cha tuzo hiyo jiji Zurich,Uswisi jana jumatatu ambapo Mreno Cristiano Ronaldo alitwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo amesema
"FIFA wanapaswa kuandaa tuzo nyingine ya pili ili moja iwe kwa ajili ya kuamua nani zaidi kati ya Messi na Ronaldo na ya pili iwe ni ya wachezaji wengine waliobaki.
"Messi na Ronaldo ni wachezaji wa kipekee sana nadhani wanapaswa kuwa na tuzo ya peke yao ambayo itakuwa haifungamani na upande wa pili yaani wachezaji wengine.
0 comments:
Post a Comment