Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajiwa kufika tamati leo usiku (2:15) kwa kuikutanisha miamba miwili ya Simba Sc na Mtibwa Sugar itakayojimwaga katika dimba la Amaan katika mpambano wa fainali.
Simba Sc inaingia dimbani leo hii kuusaka ubingwa wa tatu wa michuano hiyo huku Mtibwa yenyewe ikiusaka kwa mara ya pili.
Miamba hiyo imetinga fainali baada ya kushinda kwa tabu michezo yake ya nusu fainali.Simba iliibanjua klabu ya Polisi kwa bao 1-0 huku Mtibwa ikiing'oa Jku kwa mikwaju 4-2.
Huu ni mchezo wa pili kwa miamba hii kukutana katika michuano hii kwa mwaka huu kwani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Mtibwa ilitoka uwanjani kifua mbele baada ya kuibanjua Simba kwa goli 1-0.
MABINGWA WA MICHUANO HIYO
2007 Yanga
2008 Simba
2009 Miembeni
2010 Mtibwa
2011 Simba
2012 Azam FC
2013 Azam FC
2014 KCCA
0 comments:
Post a Comment