728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 24, 2015

    CAMPBELL OUT,PAULISTA IN ARSENAL

    London,England.

    Taarifa kutoka jiji la London kunako klabu ya Arsenal zinasema kuwa klabu hiyo hiyo imekubali kutoa ada ya £13.5m kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa klabu ya Villarreal Gabriel Paulista.

    Paulista (24) raia wa Brazil asubuhi ya leo aliripotiwa kuondolewa katika kikosi cha Villarreal ambacho leo kitashuka dimbani kuivaa klabu ya Levante ili kujua hatima ya mpango yake.

    Habari za hivi punde zinaripoti kuwa mbali ya Arsenal kukubali kutoa dau hilo pia itamtoa kwa mkopo wa miezi sita kinda wake Joel Campbell ili kuifidia Villarreal ambayo ina kipengere cha kumuuza Paulista kwa ada ya £15m.

    Paulista ambaye kiuchezaji anafanishwa na mlinzi mahiri wa Arsenal Laurent Koscienly anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya mapema wiki ijayo kabla ya kuanza kuombewa kibari cha kufanyia kazi England.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAMPBELL OUT,PAULISTA IN ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top