Zanzibar.
Klabu ya Simba imetwaa ubingwa wa kombe la mapinduzi kwa mara ya tatu baada ya kuifunga Mtibwa Sugar kwa penati 4-3.
Mpaka dakika 90 za kawaida zinaisha hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie na ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ilipoamuliwa na hatimaye Simba kushinda.
Shukrani za dhati zimuendee mlinda mlango Ivo Mapunda aliyetokea benchi muda mfupi kabla ya mchezo kumalizika na kuipa timu yake ushindi baada ya kuokoa penati ya Vincent Barnabas.
Simba ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2008,2011 na 2015.
0 comments:
Post a Comment