Guinea
Mshambuliaji Asamoah Gyan jana aliibuka shujaa baada ya kuifungia goli timu yake ya taifa ya Ghana na kuisaidia kupata pointi tatu muhimu dhidi ya timu ya taifa ya Algeria katika mchezo wa mapema wa kundi C.
Gyan ambaye alikosa mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal kutokana na kuumwa malaria aliifungua Black Stars dakika ya 92 ya mchezo baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Algeria.
Katika mchezo wa pili timu za taifa za Afrika Kusini na Senegal ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya goli 1-1.
Leo michuano miwili ya kundi D itapigwa kwa Ivory Coast kuvaana na Mali katika mchezo wa kwanza huku mchezo wa pili Cameroon ikivaana na Guinea.
0 comments:
Post a Comment