Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) itawasili Mwanza, Tanzania Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface
Wambura, Amavubi yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na
viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba.
Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya JB Belmont.Baada ya kocha Mdachi, Mart Nooij kutaja kikosi, Stars inaingia kambini keshokutwa (Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata
itakwenda Mwanza tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.
Kikosi hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo
za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kinaundwa
na wachezaji 26.
0 comments:
Post a Comment