728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, January 14, 2015

    MENDEZ:FALCAO KUTIMKA MANCHESTER UNITED

    Manchester,England.
    Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Radamel Falcao huenda akaondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu hii ni kwa mujibu wa wakala wake Mreno Jorge Mendez.
    Kauli hii ya Mendez imekuja huku kukiwa na uvumi kuwa mteja wake alikacha klabuni  siku ya jumapili baada ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 kilichoshuka dimbani na kuambulia kichapo cha bao 1-0 toka kwa klabu ya Southampton.
    Falcao bado ameshindwa kumshawishi Kocha Van Gaal kutokana na kiwango duni anachoendelea kukioonyesha klabuni hapo.
    Akiongea kuhusu
    mustakabari wa mteja wake Mendez amesema
    "Kwa sasa hatujui kinatakacho tokea siku za usoni ndani ya klabu hii.
    Tunachokijua kwa sasa ni kuwa msimu ujao Falcao atakuwa katika klabu moja kubwa sana duniani ambayo inaweza ikawa Manchester United ama yoyote ile"
    Falcao ambaye mpaka sasa amefanikiwa kupachika jumla ya mabao 3 tu katika mechi 13 alitua klabuni hapo kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja mwisho kabisa mwa dirisha la usajili akitokea klabu ya Monaco ya Ufaransa kwa ada ya £6m.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MENDEZ:FALCAO KUTIMKA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top