Morogoro,Tanzania.
Baada ya kutoka sare katika michezo miwili mfululizo ya ligi kuu hatimaye klabu ya Yanga imefanikiwa kuifunga Polisi Morogoro kwa goli 1-0 katika mchezo uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro.
Goli la Yanga limefungwa na mshambuliaji Danny Mrwanda dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya gonga nzuri za wachezaji wa safu ya kiungo.
Kipindi cha pili kilitawaliwa na kosa kosa za hapa na pale huku Polisi wakifaulu kuidhibiti Yanga na kuifanya isiwe hatari kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza.
Kesho jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa mchezo mkali wa kukata na shoka ambapo mabingwa wa kombe la Mapinduzi Simba Sport Club watavaana na mabingwa watetezi wa ligi kuu Azam FC katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment