728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, January 25, 2015

    USAJILI:COQUELIN AIGOMEA ARSENAL,POGBA ANAUZWA KWA €100M

    Depay:Vilabu vya Manchester United na Tottenham Hotsuprs vimeripotiwa kuwa katika mchuano mkali wa kuiwania saini ya winga wa klabu ya PSV Endihooven Memphis Depay ili kuimarisha vikosi vyao.Tottenham wanamtaka Depay achukue nafasi ya Aaron Lenon wakati Manchester United wanamtaka achukue nafasi ya Adnan Januzaj.

    Ings:Klabu ya Tottenham imeripotiwa kuanza jitihada za kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Burney Danny Ings 22 kwa ada ya €6.5m huku ikijiandaa kuboresha mshahara wa mshambuliaji wake Harry Kane.

    Pogba:Klabu ya Juventus imesema itakuwa tayari kumuuza kiungo wake mahiri Paul Pogba 22 ikiwa tu itapokea ofa ya €100m.Hizo ni salamu za Juventus kwa vilabu vya PSG,Manchester United na Real Madrid ambavyo kwa nyakati tofauti vimeripotiwa kumtaka kiungo huyo.

    Laporte:Klabu ya Atletico Bilbao imesema haiko tayari kumuuza mlinzi wake kinda Aymeric Laporte kwenda klabu yake ya Manchester United katika majira haya ya usajili barani Ulaya.

    Berbatov:Klabu ya QPR imetakiwa kutoa kitita cha €1.3m ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Manchester United anayejipiga kwa sasa katika klabu ya Monaco Dimitar Berbatov.

    Costa:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuongeza dau toka €20m mpaka €25m kwa ajili ya kumsajili winga wa klabu ya Shaktar Donestik Mbrazil Douglas Costa.

    Coquelin:Staa mpya wa safu ya kiungo ya klabu ya Arsenal Fransic Coquelin 23 ameripotiwa kukataa mkataba mpya aliyopewa na klabu hiyo mpaka ahakikishiwe kuwa atakuwa akicheza mara kwa mara.Hofu hiyo ya Coquelin imekuja baada ya Arsenal kusemekana kuwa iko katika mawindo ya kuinasa saini ya kiungo Ilkay Gundogan huku Arteta akiwa mbioni kuongezewa mkataba na kiungo aliye majeruhi Jack Wilshere akiripotiwa kuwa mbioni kupona enka.Mkataba wa Coquelin unaisha mwezi Juni.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:COQUELIN AIGOMEA ARSENAL,POGBA ANAUZWA KWA €100M Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top