728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 17, 2015

    VPL:SIMBA YAUA MTWARA,YANGA YABANWA

    Kocha Goran Kopunovic ameanza Ligi Kuu Bara vizuri baada ya kuiwezesha Simba SC kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

    Simba SC imeshinda mechi hiyo ikiwa ugenini leo Januari 17,2015 kwenye Uwanja wa
    Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

    Vijana hao wa Msimbazi walifunga bao kila kipindi wakianza kupitia kwa Danny
    Sserunkuma aliyeonekana kufanya vizuri katika mechi hiyo ambapo Kipindi cha pili,
    Simba SC ilikianza vizuri na harakaharaka ilifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Elius Maguli.

    Huu ni ushindi wa pili kwa Simba SC tokea ilipoifunga Ruvu Shooting mwishoni mwa mwaka jana 2014 ,ukiwa ni ushindi pekee
    chini ya Patrick Phiri halafu ikatoka sare mechi sita na kupoteza moja dhidi ya Kagera Sugar.

    Matokeo mengine

    Yanga  0-0 Ruvu Shooting
    Stand   0-1 Azam Fc
    Kagera 0-1 Mbeya City

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:SIMBA YAUA MTWARA,YANGA YABANWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top